HOSPITALI ya Regency ya jijini Dar es Salaam imeanza kufanya upasuaji wa wagonjwa wenye matatizo ya magoti na imepanga kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa wagonjwa 10 hadi 15 kila mwezi..
Daktari bingwa wa usingizi, Kim Kalange alisema upasuaji wa aina hiyo ni wa kwanza nchini na alisifu juhudi zilizofanywa na Hospitali ya Regency kuhakikisha inatengeneza chumba cha upasuaji cha kisasa.
Mwenyekiti wa Regency, Dk Rajni Kamabar alisema kwa muda mrefu Regency kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Dar es Salaam zilikuwa zikiendesha kliniki za kupima magoti na kugundua kuwa watu wengi wana matatizo hayo.
“Watu wengi wana matatizo haya lakini hawana fedha za kwenda nje kwa matibabu na nakumbuka maelekezo ya Rais John Magufuli kwamba tufanye bidii matibabu haya yafanyike hapa hapa. Hatimaye Regency kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya HCG ya India tumefanikiwa na sasa tunatangaza kwamba tumeanza kufanya upasuaji wa goti kwa mgonjwa mmoja Regency,” alisema Dk Kama