Patients to undergo knee surgery at Regency Medical Centre
748 viewsHOSPITALI ya Regency ya jijini Dar es Salaam imeanza kufanya upasuaji wa wagonjwa wenye matatizo ya magoti na imepanga kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa wagonjwa 10 hadi 15 kila mwezi..
Daktari bingwa wa usingizi, Kim Kalange alisema upasuaji wa aina hiyo ni wa kwanza nchini na alisifu juhudi zilizofanywa na Hospitali ya Regency kuhakikisha inatengeneza chumba cha upasuaji cha kisasa.
Mwenyekiti wa Regency, Dk Rajni Kamabar alisema kwa muda mrefu Regency kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Dar es Salaam zilikuwa zikiendesha kliniki za kupima magoti na kugundua kuwa watu wengi wana matatizo hayo.
“Watu wengi wana matatizo haya lakini hawana fedha za kwenda nje kwa matibabu na nakumbuka maelekezo ya Rais John Magufuli kwamba tufanye bidii matibabu haya yafanyike hapa hapa. Hatimaye Regency kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya HCG ya India tumefanikiwa na sasa tunatangaza kwamba tumeanza kufanya upasuaji wa goti kwa mgonjwa mmoja Regency,” alisema Dk Kama
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na daktari bingwa wa upasuaji wa hospitali hiyo, Phuljit Patowary wakati akizungumzia kuanza kwa huduma hiyo ya upasuaji wa magoti hospitalini hapo.
Alisema mgonjwa mmoja alifanyiwa upasuaji juzi na upasuaji huo uliokuwa wa mafanikio ulichukua saa moja na kwamba hiyo ni fursa kwa wagonjwa wengi ambao walikuwa wakienda nje ya nchi kutibiwa magoti.
“Kuna wakati hata Rais John Magufuli alisema matibabu kama hayo yafanyike hapa Tanzania sasa Regency ndiyo imeanza kutekeleza maoni ya Rais wetu na Watanzania waliokuwa wakisumbuka kwenda nje ya nchi kwa matibabu haya sasa wataokoa fedha zao,” alisema.
Aidha, alisema wamechukua baadhi ya madaktari kutoka Hospitali mashuhuri duniani ya HCG iliyoko mji wa Ahmedabad nchini India ambao wako kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kuendesha upasuaji huo.
Daktari bingwa wa usingizi, Kim Kalange alisema upasuaji wa aina hiyo ni wa kwanza nchini na alisifu juhudi zilizofanywa na Hospitali ya Regency kuhakikisha inatengeneza chumba cha upasuaji cha kisasa.
Mwenyekiti wa Regency, Dk Rajni Kamabar alisema kwa muda mrefu Regency kwa kushirikiana na Klabu ya Lions ya Dar es Salaam zilikuwa zikiendesha kliniki za kupima magoti na kugundua kuwa watu wengi wana matatizo hayo.
“Watu wengi wana matatizo haya lakini hawana fedha za kwenda nje kwa matibabu na nakumbuka maelekezo ya Rais John Magufuli kwamba tufanye bidii matibabu haya yafanyike hapa hapa. Hatimaye Regency kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya HCG ya India tumefanikiwa na sasa tunatangaza kwamba tumeanza kufanya upasuaji wa goti kwa mgonjwa mmoja Regency,” alisema Dk Kamabar